
Ndizi ni mojawapo ya tunda lenye ladha nzuri na limekuwa likipendwa na watu kutokana na ladha yake hiyo.
Aidha ndizi imekuwa likisifika sana kwa faida zake za kiafya, japokuwa
si wengi wanazifahamu kwani wengi hulichukulia kama tunda la kawaida tu.
Hata hivyo ni vyema ikafahamika kuwa tunda hili ni nzuri sana kwa
wanaume kutokana na kuwa na uwezo mzuri wa kuboresha masuala ya uzazi
kwa jinsia hiyo.
Ndizi ni nzuri sana katika kuboresha mbegu za kiume na kuongeza uwezo wa
kufanya tendo hilo vizuri na kwa muda, hivyo ni vizuri kujenga
utaratibu wa kula tunda hili mara kwa mara ili kupata faida zaidi.
Ndani ya ndizi kuna virutubisho muhimu kama 'potassium' ambayo husaidia sana kuongeza kiwango cha mbegu kwa wanaume.
Pamoja na hayo ikiwa utaona unamuda mrefu kwenye ndoa na hujafanikiwa
kupata mtoto ni vizuri ukafanya utaratibu wa kuwaona wataalam kwa
ushauri zaidi