BANDA MEDIA BLOG

SAMIA SULUHU AWATAKA MA SECRETARY NCHINI KUZINGATIA MAADILI YA KAZI


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na Makatibu Mahsusi kwenye mkutano wao wa kila mwaka unaofanyika mjini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akizungumza na makatibu Mhtasi hao
Mwenyekiti wa chama cha makatibu mahsusi nchini Zuhura Maganga akiongea kwa furaha wakati wa mkutano huo

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki na Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Maganga [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]


Makatibu Mahsus wakifuatilia jambo wakati mkutano wao wa mwaka ukiendelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete



Makamu wa Rais akapata zawadi Baada ya kuwafungulia mkutano huo ulioambatana na mafunzo mbalimbali





Na John Banda, Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameaagiza kada ya wahazili nchini marufu makatibu mahsusi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili kuacha  tabia ya kutoa siri za serikali kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na kwamba serikali haitowavumilia kwa kukiuka kiapo cha maadili ya viongozi wa umma

Ni katika  mkutano wa Tano wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania unaofanyika hapa mjini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete ambapo makatibu mahsusi ama Secretary  kwa lugha ya kimombo wanatajwa kuwa kiungo muhimu katika ofisi mbalimbali za umma ambapo wamekuwa wakisaidia shughuli mbalimbali kwa viongozi 
 
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uadilifu na uaminifu ni njia pekee ya kuaminiwa na viongozi wao hivyo ni muhimu kwa makatibu mahsusi nchini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa katika maeneo yao ya kazi.
"Kuvujisha Siri ni kosa la Kisheria na ni kinyume cha maadali ya msingi ya kada na taaluma yenu na madhara yake ni makubwa zaidi ikiwemo kuchukuliwa hatua za kisheria, 

 sisi wanawake tunapenda kula ubuyubuyu tunaupenda mara mbili kuula na kiha kuutema lamsingi hapa ni vizuri ukatema na kuuficha mtu asiuone", alisema

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amesema Serikali inafanyia kazi baadhi ya kero zinazowakabili makatibu mahsusi ikiwemo kuboresha maslahi ya kada ya uhazili nchini.

 Awali akizungumza na kada ya wahazili Mwenyekiti wa chama cha makatibu mahsusi nchini Zuhura Maganga akaeleza changamoto zinazoikabili sekta hiyo muhimu nchini ikiwemo masirahi duni ikiwa ni pamoja na mishahara midogo, baadhi ya waajili kutotambua mafunzo yanayotolewa na watumishi wa Umma na kutopandishwa vyeo

Nje ya ukumbi wa mkutano huo BANDA BLOG  ilizungumza na baadhi ya makatibu mahsusi  kutoka maeneo mbalimbali nchini ambapo walidai kuwa kwa sasa kada hiyo imekuwa ikilinda maadili ikiwemo kuepuka utoaji siri za serikali na kuepuka mialiko toka kwa mabosi wao wasiojiheshimu
 
Mkutano huo wa makatibu mahsusi hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Umoja kwa maendeleo ya Taaluma

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG