
Kitendo cha Star TV kurusha matangazo ya mahojiano yenye mvurugano
hakivumiliki. Mahojiano yasiyo na uwiano yalilenga kudhalilisha.
Yalilenga kumuanika na kumfanya kuaibika RC wa Dar, Daudi Albert Bashite
aka Paul Makonda.
Mahojiano yamemuacha Bashite peupe na akiwa amesawajika kiuhakika. Ubovu
wa majibu; kukosa umakini na kubabaikababaika kwa Bashite kumemuacha
Bashite katika hadhara ya hasara. Mahojiano yamekuwa ugonjwa wa jino.
Maumivu makali kama kabali.
TCRA fungieni Star TV na wanyang'anyeni leseni. Ni katika kumlindia
heshima Bashite. Mahojiano yamekoleza manjano kwenye tuhuma. Tuhuma za
kubuma katika kusoma. Mahojiano yalipaswa kupangwa na kupangika
kiuhakika. Si vile. Hayakufaa.
Nafasi haikutumika,nanasi limeharibika. Majivuno yameleta miguno ya
kukataa kuambiwa uongo hata kwa hongo. Bashite ameumbuka. Bashite
amedhalilishwa. Nani aliwatuma Star TV?
Rambirambi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea,Ruvuma)
Chanzo Jf
Tags
Paul Makonda