Baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na weusi sehemu za makwapa, hali
ambayo huwakwaza hasa zaidia kinadada na kujikuta wakishindwa kuvaa
baadhi ya mavazi hasa yale yenye mikono mifupi kwa kuhofia hali hiyo.
Leo nimekuletea hii mbinu ya kutumia ganda la chungwa kumaliza weusi wa sehemu za kwapani.
Unachotakiwa kufanya ni kukamua maji ya ganda la chungwa (yale ambayo
yakiingia machoni huuma) weka maji hayo kwenye kikombe kisha changanya
na asali kijiko kimoja kidogo kisha paka mchanganyiko huo sehemu
iliyoathirika. Fanya zoezi hili kwa wiki mbili ili kupata matokeo
mazuri.
