IGP Simon Sirro amewaonya wahalifu wanaojishughulisha na mauaji mkoani
Pwani kuacha mara moja kwani ndani ya muda mfupi ataenda kuwafichua kwa
kutumia vyombo vyake vya dola ili kulinda amani ambayo imepotezwa na
kikundi cha watu wachache.
IGP Siro ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wanahabari leo jijini
Dar es salaam na kusema kuwa haki lazima iende kutoa majibu ya watu
wanaofanya mauaji maeneo ya kibiti, mkuranga, Ikwiriri kwa ndani ya
muda mfupi huku akiongeza hakuna sababu ya watu wema kufanyiwa ubaya na
kama jeshi ni wajibu kuilinda amani.
"Hakuna haja ya watu kufanya ukatili na ubaya kwa watu wasiostahili.
Sisi tutawajibu ubaya wanaofanya ubaya. Watanzania pamoja na vuiongozi
wangu wanataka maji ya nani anayefanya haya mauaji, lakini tayari
tumeshapata kujua ni kikundi cha watu wachache niwahakikishie mimi
pamoja na vyombo vya dola tutawapatia majibu ndani ya muda mfupi"- IGP
Sirro aliwaambia wanahabari.
Pamoja na hayo katika mkutano huo na wanahabari IGP Sirro amewataka
wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuachana na biashara hiyo haramu
kwani hailipi kama jinsi wanavyofikiria na badala yake itawahamisha
uraiani na kuwatenga na familia zao kutokana na jinsi watakavyo
shughulikiwa na sheria za nchi.
Sambamba na hayo Sirro ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kuacha
kujichukulia sheria mikononi kwa makosa madogo madogo yanayojitokeza
mitaani na kwamba ni kinyume cha sheria za nchi nawote wanaofanya hivyo
ameahidi kuwashughulikia kwa sheria.
"Kila mtu atahukumiwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Kuna wale watu
wanajidai kwamba wanahasira kali hadi kufikia kumuua mtu aliyeiba kuku,
niwaambie tu kuku hana thamani ya mwanadamu na hao wenye hasira kali
nitaenda nao sambamba kwa sababu imefika hatua eti vifo vya silaha ni
vichache kuliko vya hasira kali" - aliongeza IGP Sirro
Tags
IGP SIRRO