Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa Mkutano wa 10 wa
Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar
es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo
Kassim Majaliwa, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza Hilo kutoka Sekta Binafsi
(TPSF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati
Tendaji wa TBNC Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Ajira, Vijana, Bunge na Watu wenyeulemavu Jenister Muhagama.
Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti
wa Kamati Tendaji wa TBNC Balozi John Kijazi akitoa utambulisho wa
wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakati wa Mkutano
wa 10 wa Baraza hilo na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la
Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ndiye
Mwenyekiti wa Baraza hilo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo leo
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwenyekiti
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) Dkt. Reginald
Mengi wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania
(TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri
Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa.
Rais wa Taasisi ya Wakuu wa
Makampuni CEO Round Table Ally Mfuruki akisalimiana na Mwenyetiki wa
Taasisi za Kibenki ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB
Dkt. Charles Kimei wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara
Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye akiteta jambo na Gavana wa Benki
Kuu (BOT) Profesa Benno Ndulu wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la
Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa
10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada
wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Charles Mwijage akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa
Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na
uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene
akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara
Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa
10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana
na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) Dkt. Reginald Mengi akiteta jambo na Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) Mhandisi Raymond
Mbilinyi (katikati) na Mkurugenzi wa TPSF, Godfrey Simbeye.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais –
TAMISEMI Mhandisi, Mussa Iyombe akielezea jambo mbele ya Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospether Muhongo (katikati), Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge na Waziri wa Maliasili na Utalii
Profesa Jumanne Maghembe (kushoto).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakati wa Mkutano
wa 10 hilo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto
ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu
Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TBNC, Balozi John
Kijazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana,
Bunge na Watu wenyeulemavu Jenister Muhagama.
……………………
Na Jacquiline Mrisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini
kujitathmini, kurekebisha makosa yao pamoja na kutumia fursa mbalimbali
zinazotolewa na Serikali badala ya kuilalamikia kuwa haiwasaidii.
Rais Magufuli ameyabainisha hayo
wakati akiongea na wafanyabiashara wa sekta binafsi katika mkutano wa 10
wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika leo Ikulu Jijini Dar
es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa tenda
mbalimbali za ujenzi wa miundombinu zimekuwa zikitolewa na Serikali mara
kwa mara lakini wakandarasi nchini wamekuwa hawazitumii fursa hizo na
matokeo yake zinatolewa kwa wakandarasi kutoka nchi zingine.
“Serikali inatangaza tenda nyingi
za ujenzi wa miundombinu na kwa kiasi kikubwa huwa inawalenga
wakandarasi wa ndani kuliko wanaotoka nje lakini wakandarasi wetu
wamekuwa hawazitumii fursa hizo, Serikali itachoka kuwabeba hivyo wakae
wajitathmini,” alisema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa wakandarasi
wanatakiwa kuungana na kufanya kazi kwa pamoja ili waweze kupata tenda
zinazotolewa na Serikali kwa urahisi pia amewataka wawe wazalendo katika
upangaji wa bei za kazi zao.
Akitoa mfano wa kukosa uzalendo,
Rais Magufuli amesema kuwa wakandarasi wa hapa nchini walipoombwa kutoa
bei za ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walitaja kiasi
cha shilingi kati ya bilioni 150 na 200 wakati Wakala wa Majengo (TBA)
waliyajenga kwa bilioni kumi tu.
Aidha, Rais Magufuli amewapongeza
wafanyabiashara wa sekta binafsi kwa kushirikiana na Serikali katika
kujenga uchumi wa viwanda na kuwahakikishia kuwa Serikali iko pamoja nao
katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe.
Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa taasisi zinazohusika na huduma za
bandari zikiwemo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango
Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuanza kutoa huduma
zao kwa saa 24.
“Tumeamua kufanya hivyo ili
kurahisisha huduma kwa wafanyabiashara kwani wamekua wakipata shida kwa
kutumia muda mrefu kupata huduma katika bandari yetu, nafikiri njia hiyo
itachochea wafanyabiashara kuwekeza zaidi”, alisema Mhe. Majaliwa
Ametoa rai kwa wafanyabiashara wa
sekta binafsi kuwekeza kwenye kilimo kwani maendeleo ya ujenzi wa
viwanda unategemea malighafi zinazotokana na kilimo.
Aidha Majaliwa alisema Serikali
imekusudia kupanua wigo katika sekta ya kilimo kwa kuleta zana bora za
kilimo, kuendelea kupunguza kodi katika mazao pamoja kuiwezesha Benki ya
Kilimo kuendelea kutoa mikopo kwa wingi.
Nae, Mwenyekiti wa Taasisi ya
Sekta Binafsi, Dkt. Reginald Mengi ameipongeza Serikali kwa kutekeleza
ahadi mbalimbali walizojiwekea zikiwezo za elimu bure, ujenzi wa
miundombinu, ununuzi wa ndege pamoja na kukaa na wananchi na wadau
mbalimbali kusikiliza na kutatua changamoto zao,
“Ushiriki wa wadau kwenye kikao
hiki ni muendelezo chanya wa mahusiano mazuri kati ya Serikali na sekta
binafsi, ninaamini majadiliano haya yatatatua changamoto za
wafanyabiashara wa sekta binafsi”,alisema Dkt. Mengi.