Nimepata habari kuwa kuna ufisadi mkubwa umefanyika ndani ya CHADEMA kwa
kutumia fedha za ruzuku. Kwamba, T. Shirt moja iliyovaliwa wakati wa
Kamati Kuu na Baraza Kuu la CHADEMA lililofanyika Doeoma hivi karibuni
imetengenezwa kwa shilingi 120,000 na kwamba kila aliyevaa ametakiwa
kulipa nusu ya bei na nusu nyingine kimegharamia chama.
Taarifa hizo zinasema kuwa baadhi ya wajumbe wamegoma kulipa gharama
hizo kwa madai kuwa bei ni kubwa mnooooo! Inadaiwa pia kuwa wajumbe
wengine waligoma kuzivaa ili wasiwe sehemu ya ufisadi huo.
Kama habari hizi ni za kweli basi kale kaugonjwa kalikokimbia CCM kametaga mayai CHADEMA
Chanzo JF
Tags
CHADEMA