
Ukiacha masuala ya kisiasa na ukamuuliza swali Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi (CUF) taifa, Prof. Ibrahim kuwa ni shabiki wa Klabu gani ya
mpira wa miguu Duniani, bila kupapasa macho atakujibu ni Arsenal.
Lipumba amesema yeye ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal, licha ya klabu
hiyo ya England kutotwaa mataji makubwa kwa muda mrefu lakini bado
haipunguzi mapenzi yake kwa klabu hiyo ya Ligi kuu England.
“Naishabikia Arsenal japo kuwa haifanyi vizuri, lakini ndio timu yangu
ninayoipenda,”Alijibu Prof. Lipumba kwenye kipindi cha Clouds 360 cha
Clouds TV leo asubuhi alipoulizwa ni klabu gani ya mpira wa miguu
anaishabikia.