Mdhamini wa Taasisi ya
Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini
Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za
kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru
wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. 9PICHA NA
RICHARD MWAIKENDA)
Mdhamini wa Taasisi ya
Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini
Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za
kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru
wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. Kutoka kulia
ni Rais wa taasisi hiyo, Ali Akkiz na Mshauri wa masuala ya Habari,
Felix Kaiza.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mshauri wa Masula ya Habari,
Felix Kaiza akielezea umuhimu wa wamiliki wa vyombo vya habari kuweka
utaratibu wa mafunzo ya ndani (In House Training) kwa waandishi wa
habari ili kuinua weledi pia alishauri kuwepo na Exchange Program kati
ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchini jambo ambalo huwaongezea
uwezo wanahabari.
Mtangazaji wa Kituo cha
Televisheni cha Chanel Ten, Esther Zaramula akielezea kwenye mjadala huo
jinsi alivyonufaika na mpango wa kubadilishana uzoefu
Habib Miradji akisisitiza jambo
wakati wa mjadala huo ambapo alifafanua zaidi umuhimu wa wanahabari
kuandika habari kwa kufuata maadili na kusimamia kwenye ukweli.
Pia katika kongamano hilo
waliwaasa wanahabari kutojiingiza katika mkumbo wa kuingizwa mifukoni
mwa wanasiasa na matajiri kwa kuandika habari za kuwasifia wao badala ya
maslahi ya wananchi.
Mwandishi wa habari, Ezekiel
Kamwaga akielezea umuhimu wa wanahabari kujiendeleza kielimu pamoja na
vyombo vya habari kubadilika kwa kwendana na kasi ya mabadiliko ya
kizazi hiki cha maendeleo ya teknolojia ya habari.
Rais wa taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Ali Akkiz aktoa shukrani kwa wanahabari walioshiriki kwenye mjadala huo uliofanikiwa.
Tags
Amani ya Nchi