Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amemtaka mbunge wa kwimba Mhe.
Shannif Mansuri alipe kiasi cha shilingi million 529 ambayo ni
malimbikizo ya Kodi ya pango la ardhi tangu mwaka 2010 ndani ya siku
saba.
Waziri Lukuvi amesema hayo
alipokuwa katika ziara yake Mkoani Mwanza wilaya ya Nyamagana na kufanya
ukaguzi katika mfumo wa kodi ambapo aligundua watu wenye madeni makubwa
ya pango la ardhi akiwemo mbunge huyo.
Baadae ya kugundua hilo
ikamlazimu kutoa agizo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la
wilayani Nyamagana kuhakikisha mbunge huyo analipa deni hilo ndani ya
siku saba kinyume na hapo ni kupigwa mnada eneo lake au kufutiwa hati
yake.
Aidha, katika ukaguzi huo pia
aligundua urasimu na uzembe wa watendaji wa jiji la Mwanza katika sekta
ya ardhi, ambapo ameona kwenye baadhi ya mafaili kuwepo kwa watu
wanaofuatilia hati zao zaidi ya miaka mitano bila mafanikio. Hivyo,
Waziri Lukuvi alichukua hatua za kupiga simu kwa mmoja wa watu hao ili
kuthibitisha ni kwa nini hajapewa hati ambapo aligundua kuwa amekuwa
akizungushwa na watumishi hao. Hapo alitoa agizo kwa watendaji hao kutoa
hati kwa Mama huyo na wengine wote haraka iwezekanavyo.
Mh. Lukuvi amewaeleza watendaji
wa jiji la Mwanza mbele ya Mkuu wa Mkoa John Mongella kufuatilia kwa
karibu mfumo wa kodi ya pango la ardhi, na utoaji wa hati kwa wananchi
kwa kuwa masuala hayo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, sababu huongeza
pato la serikali hivyo kuinua uchumi wa nchi.
Tags
Kodi ya ARDH