
Staa asiyechuja wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’
amefunguka kuwa katika maisha yake ya kimuziki, hajawahi kuwa na nidhamu
ya uoga kama ambavyo baadhi ya watu wanavyomponda.
Roma alifunguka hayo wikiendi iliyopita alipokuwa akipiga stori na Uwazi
Showbiz kufuatia maneno kutoka kwa mashabiki wake kuwa muziki wake
utachenji kutokana na hofu, tofauti na alivyozoeleka kuwa na mashairi
makali ya kuikosoa serikali.
“Kamwe sijawahi kuwa na nidhamu ya uoga maishani mwangu, kinachotokea
kwa sasa ni mabadiliko tu ya muziki wangu, siwezi kuimba siasa kila
siku, ukweli ni kwamba kwa kuimba siasa kila siku zinafanya muziki wangu
usiwe wa kimataifa na uwe ni muziki wa ndani,” alifunguka Roma ambaye
bado hajapona makovu aliyoyapata
Tags
Roma