
Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja wa Pakistani amejikuta
akifanya ‘fungate’ maarufu kwa lugha ya kigeni kama honeymoon peke yake
bila mumewe, tukio linalopaswa kufanywa na wanandoa.
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Huma Mobin alifunga ndoa miezi
kadhaa iliyopita na mumewe, Arsalan Sever na wawiwili hao walipanga
kwenda kufanya fungate lao nchini Ugiriki, wakiamini ni sehemu
watakayokula raha zaidi.
Hata hivyo, hali haikuwa kama walivyopanga baada ya mume wa Huma
kunyimwa kibali cha kuingia nchini Ugiriki (Visa), huku mwanamke
akikubaliwa kuingia nchini humo.
Kwamuhibu wa mtandao wa BuzzFeed, mwanamke huyo alijikuta nchini Ugiriki
peke yake akilia usiku kucha, lakini aliuambia mtandao huo kuwa mama
mkwe alimtia moyo na kumtaka ale raha peke yake kadiri awezeka, “make
the best of it.”
Picha na jumbe alizoweka mtandaoni mwanamke huyo zilisababisha kupata
umaarufu mkubwa na kuzungumziwa na vyombo vikubwa vya habari kama BBC na
CNN, hadi wawili hao walipokutana tena.