
Napenda kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa uzalendo na
mapenzi ya dhati anayoonyesha kivitendo kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla
kwa kuhakikisha analinda rasilimali, Mali, haki na maslahi.
Hivi karibuni Rais Magufuli alizuia makontena 277 yenye mchanga wa
madini kusafirishwa kwenda nje ya nchi na kuunda kamati kuchunguza
hasara au faida tuliyokuwa tukiipata Watanzania kutokana na kusafirisha
mchanga huo ambapo kamati imewasilisha taarifa ya awali imeonyesha
thamani ya makontena hayo 277 ni Tsh. Bilioni 112.1 kumbe thamani halisi
ni Tsh. Trilioni 1.44. Taarifa hiyo imeonyesha hayo makontena tu
tulikuwa tumepoteza zaidi ya Tsh. Bilioni 829.4 ambapo kwa mwaka mmoja
tu tulikuwa tukipoteza Trilioni 25 ambayo Serikali ilikuwa haipati hata
senti moja.
Kupitia mchanga huo tu tulikuwa tukiibiwa hivyo kwa takribani miaka 18
huku tukipoteza Tsh. Trilioni 829.4 sawa na bajeti ya miaka 26 ya Tsh
Trilioni 32 kwa kila mwaka.
Tunapoteza pesa hizo huku tukiangalia mahospitali hayana madawa,
miundombinu mibovu, mishahara haikidhi, tunakopa kukamilisha bajeti ya
nchi maumivu ambayo hatukustahili kabisa kuyapata sisi Watanzania.
Ahsante sana Rais Magufuli kwa kuonyesha uzalendo wa kuzuia unyonyaji na
uhujumu uchumi huu wa kikatili uliokuwa ukiendelea nchini. Ni viongozi
wachache sana Afrika waliosalia wenye kariba ya uzalendo kama alionao
Rais Magufuli.
Huu ni mwendelezo wa uzalendo wa kivitendo unaoonyesha na Rais Magufuli.
Tukumbuke ni Rais Magufuli huyu huyu anasimamia vyema upotevu wa mapato
bandarini, kuzuia matumizi ya ovyo Serikalini ya kodi za Wananchi kwa
kufuta safari za nje, kulipana posho zisizo na tija na kupunguza
matumizi ya kawaida kwa kuongeza fedha zaidi kwenye matumizi ya
kimaendeleo.
Kiukweli ninaiona Tanzania mpya ikijengwa na uzalendo alionao Rais
Magufuli kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla. Watendaji, viongozi na
Wananchi yatupasa tuige Uzalendo wa Rais wetu mpendwa Dk. John Pombe
Magufuli kwa kuungana nae kupambana na wahujumu uchumi wa nchi yetu.
Rais Magufuli fanya uliyotumwa na wanyonge usiogope wanaojiita
wachambuzi ambao kila kitu hukuchambua kinyume, hao ni changamoto ya
wewe kusonga mbele!
Tunakuombea Rais Magufuli ulinzi, Baraka, hekima na busara zaidi toka kwa Mwenyezi Mungu.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Dk. Magufuli.
Na Emmanuel J. Shilatu
25/05/2017
0767488622
Tags
RAIS MAGUFULI