Naibu
Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Dkt.Hamisi Kingwangalla akiongea na Mzee Maige ambaye amelazwa kwenye
chumba cha kitengo cha dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ambapo asubuhi ya leo mzee huyo alihamishiwa hapo kwa uchunguzi wa afya
na matibabu zaidi kutoka hospitali ya Rufaa ya Amana.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya dharura Renatus Tarimo(kushoto) akimueleza Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto jinsi
walivyompokea na kumuhudumia kwenye kitengo chao na hali ilivyo hadi
sasa,Dkt. Tarimo amesema hali ya Mzee maige inaendelea vizuri na
wameshamfanyia uchunguzi wa awali na wanaendelea na uchunguzi zaidi
Mkuu
wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma
Mfinanga (katikati) akimueleza jambo Naibu Waziri Dkt. Kingwangalla mara
baada ya kutoka kwenye chumba alicholazwa Mzee Maige.Mzee Maige au kwa
jina maarufu anajulikana kama Ngosha ndiye aliyebuni Nembo ya Taifa
ambayo inatumika hadi sasa nchini.
Naibu Waziri Dkt.Kingwangalla
akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dkt.Mfinanga(kulia) mara baada ya kumjulia hali Mzee
aliyebuni nembo ya Taifa Mzee Francis Maige kwenye ofisi ya mkurugenzi
wa Hospitali hiyo,kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Profesa
Laurence Maseru
Mzee
Maige akiongea na Naibu Waziri,Wizara ya Afya,maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Kingwangalla(Picha na Catherine
Sungura-WAMJW)
Tags
AFYA