
Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo
imewasilisha bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika
kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni
za bunge nje na ndani ya bunge hilo.
Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge
kosa lililofanywa na Paul Christian Makonda na Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru, Alexander Mnyeti.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili
wamesamehewa kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la
Tanzania.
Aidha, Kamati ya Maadili ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa lugha ya kudharau mamlaka
ya bunge.
Pia Kamati ya Maadili ya Bunge imemuadhibu Mbunge Halima Mdee
kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia kwa kudharau
mamlaka ya bunge.
Hata hivyo, Bunge limeazimia kumsamehe mbunge huyo baada ya Wabunge wa pande zote kumuombea msamaha .
Katika hatua nyingine,Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya amepewa
karipio kali na Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kosa la kudharau Mamlaka
ya Spika wa Bunge.