Ushindi wa magoli 2-1 walioupata
Yanga dhidi ya Kagera Sugar unawafanya wafikishe pointi 62 sawa na Simba
lakini Yanga wanarejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi
kutokana na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Yanga wamecheza mechi yao ya 27
mechi moja nyuma ya Simba ambayo tayari imeshacheza mechi 28 hadi sasa
na kubakiwa na mechi mbili kabla ya ligi kumalizika.
Yanga walifunga goli la kwanza
kupitia kwa Simon Msuva aliyeunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na
Geoffrey Mwashiuya dakika ya 38 kipindi cha kwanza. Mbaraka Yusuph Abeid
akaisawazishia Kagera Sugar dakika ya 45+5 baada ya makosa ya beki
Kelvin Yondani kushindwa kuutuliza Mpira na kufanya timu hizo kwenda
mapumziko zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1.
Obrey Chilwa akaifungia Yanga goli
la ushindi dakika ya 58 kwa kuunganisha krosi ya Haruna Niyonzima na
kuihakikishia Yanga ushindi pamoja na pointi tatu muhimu.
Kagera Sugar imefungwa na Yanga
mechi zote (mbili) za msimu huu na kuichangia Yanga pointi sita, mechi
ya mzunguko wa kwanza Kagera Sugar ilikubali kichapo cha magoli 6-2
kwenye uwanja wa Kaitaba kabla ya leo kufungwa 2-1 kwenye uwanja wa
taifa.
Tags
yanga