Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza nas Wananchi wa Shehia
tatu za Bungi, Ubago na Tunguu wakati wa kukabidhi vifaa kwa ajili ya
shehia hizo tatu kwa matumizi ya Kijamii wakati wa shida na raha, Vifaa
walivyokabidi majiko ya gesi 3, sinia 800 mitungi ya gesi 6 na
mabusati. kwa ajili ya matumizi yao katika shughuli za kijamii, hafla
hiyo ya makabidhiani imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Wilaya ya Kati
Unguja. Na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja.
Mbunge wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mhe. Khalifa Salim Suleiman akizungumza na wananchi wa jimbo
lake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi ya
shughuli za kijamii katika jimbo lao ikiwa ni kutimiza ahadi kwa
wananchi wa jimbo lao walioitowa wakati wa kampeni ya uchaguzi.hafla
hiyo imefanyika katika tawi la CCMTunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la
Tunguu wakikabidhi vifaa mbalimbali waliohidi kwa wananchi wa jimbo lao
wakikabidhi vifaa hivyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg
Ramadhan Abdallah na Uongozi wa jimbo hilo, hafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa Tawi la CCM Tunguu Unguja. wakikabidhi mabusati na
sinia.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la
Tunguu Zanzibar wakikabidhi majiko ya gesi kwa ajili ya shia tatu kila
shehia imepata jiko moja na mitungi ya gesi miwili. na sinia 200, kwa
ajili ya matumizi ya kijamii katika shehia zao.Hafla hiyo ya
makabidhiano imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Unguja.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la
Tunguu wakikabidhi sufuria kwa Uongozi wa Jimbo kwa ajili ya matumizi
ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata sufuria mbili kubwa.
Mbunge na Mwakilishi wa
Jimbo la Tunguu wakikabidhi mitungi ya gesi kwa Uongozi wa Jimbo kwa
ajili ya matumizi ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata
mitungi miwili ya gesi mikubwa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za
kijamii katika jimbo lao zilizotolewa na viongozi hao..
Mwenyekiti wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar Mzee Khatib Ramadhani akitowa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge
kwa msaada wao huo kwa ajili ya kuwajali wananchi wa jimbo lao kwa
msaada huo na kuahidi kuutumia kwa malengo yaliokusudiwa katika shughuli
za kijamii katika shehia husika za jimbo hilo.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu
Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali dhamira
wa msaada huo kwa wananchi wa jimbo lao kuweza kuwasaidia katika
matumizi yao ya shughuli za kijamii zinazotokea kwa wananchi hao ili
kuweza kuvitumia kupunguza gharama za kukodi vifaa hivyo.
Imetayarishwa na OthmanMapara,zanzinews.com.
email. othmanmaulid@gmail.com.