Mchango wa Mbunge wa Kuteuliwa(CCM), Salma Kikwete kuhusu kupinga
wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo
jana ulizua gumzo bungeni kutokana na wabunge kugawanywa na suala hilo.
Hali hiyo ilijitokeza wakati wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya
bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha
2017/18 bungeni jana.
Salma amesema anapinga suala la watoto wanaopata ujauzito shuleni
kuendelea na masomo kutokana na mila, desturi, dini na mazingira.
Ameitaka Serikali kutafuta njia nyingine ya watoto hao kupata elimu badala ya kuwaruhusu kuendelea na masomo.
Akitoa taarifa yake kwa mchangiaji Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally
Keissy alitaka mbunge yeyote ndani ya Bunge ambaye alianza kushiriki
mapenzi akiwa shuleni atoe ushuhuda bungeni kama aliweza kuendelea
vizuri kimasomo.
Amesema anaunga mkono wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo
Tags
MAMA SALMA KIKWETE
