Wakazi wa Barabara ya Iloganzala Jijini Mwanza jana walipigwa butwaa
baada ya mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga using'olewe.
Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe
ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu.
Katika eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Shughuli ya kuung'oa mti huo aina ya mwembe leo imeendelea ikiwa ni
siku ya pili ya kukabiliana na mwembe huo na hatimaye wamefanikiwa
kuung'oa huku mamia ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la ajabu
Tags
MAAJABU
