Abou Coulibaly atachezesha mchezo
wa pili wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Serengeti Boys ya Tanzania
na Angola utakaofanyika Uwanja wa l’Amitie kuanzia saa 11.30 jioni kwa
saa za Tanzania.
Mwamuzi Coulibaly atasaidiwa na
Mamady Tere wa Guinea na Attia Amsaad wa Libya wakati mwamuzi wa akiba
atakuwa Mohamed Maarouf wa Misri huku Kamishna akiwa ni Ismael Locate wa
Reunion.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys,
Bakari Nyundo Shime amesema kwamba ameiona Angola ikicheza na Niger
katika mchezo wa kwanza uliofanyika mara baada ya mchezo wa Serengeti na
Mali.
“Utakuwa ni mchezo wa ushindani.
Nasi tunakwenda kushindana. Matokeo ya awali ya sare kwa timu zote mbili
yanafanya mchezo huu kuwa mgumu kwa kundi B.
“Angola ni wa kuchungwa sana. Kwa
sababu walipocheza na Niger waliweza kusawazisha mabao mawili kipindi
cha pili. Hii inaonesha kuwa ni wepesi wa kusoma makosa yao na
kujirekebisha.
“Ila kikosi changu kiko imara,
nikiamini kwamba kesho nitapata matokeo mazuri. Watanzania waendelee
kutuombea. Tutafanikiwa,” amesema Shime maarufu kwa jina la Mchawi
Mweusi.
Tags
SERENGETI BOYS