Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na
wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika
mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es
Salaam,jana.
**********************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo,amesema hakuna mtu anayeweza
kukinunua Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa ni Chama kikubwa kilichoanzishwa
na waasisi makini.
Amesema
waasisi walizingatia misingi ya haki umoja na mshikamano ,wakaondoa
dhulma, chuki na ubaguzi wa kila aina hivyo si rahisi mtu kufanya
biashara na CCM.
Mpogolo
alisema hayo jana alipozungumza na viongozi na wanachama wa CCM katika
majimbo ya Temeke na Mbagala jijini Dar es Salaam,ikiwa ni mwendelezo wa
ziara zake za kuimarisha Chama.
Alisema
CCM inaendesha shughuli zake kwa uhuru na itahakikisha uchaguzi wake
unafanyika kwa haki pasipo kuingilia na wanachama wenye tabia ya kununua
madaraka.
Mpogolo
aliwaagiza watendaji wa Chama na jumuiya kusimamia uchaguzi unaendelea
kufanyika kwa haki bila kuwashinikiza wanachama kwa kuwa wanawafahamu
viongozi wanaowataka.
“Hatutaki
vurugu CCM, tunapenda amani,umoja na mshikamano. Wenye ni ya kutumia
uchaguzi huu kupanga mitandao yao, wataambulia patupu,watatumia fedha na
uongozi hawatapata,”alisema.
Aliwaonya
wenye nia ya kuwagawa wanachama kwa misingi ya udini na ukabila kuacha
mara moja kwa kuwa CCM haina dini wala kabila na wanachama wako huru
kuchagua kiongozi anayefaa bila kujali dini wala kabila yake.
Akizungumzia
mabadiliko ndani ya Chama, Mpogolo alisema yanalenga kurejesha nguvu ya
Chama kwa wanachama ,kwa kujenga mashina yenye nguvu huku balozi akiwa
jukumu kubwa kuisimamia serikali.
Alisema
mabadiliko hayo yanataka kwenye shina kuwe na wanachama 50 hadi 150 ili
kuongeza nguvu ya Chama . Aliwataka wanachama na viongozi kujenga
umoja,upendo ili wawe kivutio kwa wengine wajiunge na CCM.
“Katika
ziara yangu nilifika Namtumbo nikakaribishwa nyumbani kwa balozi, akiwa
na wanachama wake 50,akanieleza kwamba wana kero ya maji
,nikamsimamisha diwani aeleze mipango ya kutatua kero hiyo.Pale ndio
niliona nguvu ya balozi,”alisema.
Wakizungumza
baada hotuba hiyo ,baadhi ya wanachama na viongozi walimshukuru Mpogolo
kwa ziara hiyo iliyosheheni mikakati ya kukijenga Chama na kuwaonya
watendaji jambo ambalo.
Katibu
wa CCM wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Saad Kusilawe, alisema Chama
kimejipanga vizuri kukomboa majimbo yote ya mkoa huo, hivyo ziara yake
imeongeza nguvu kwenye mikakati inayoendelea kutekelezwa.
Alisema
kutokana na ziara hiyo ,anaamini uchaguzi utafanyika kwa amani na
utulivu bila malalamiko wala upendeleo na kila ngazi itapata viongozi
bora watakaoshirikiana na wanachama kukivusha Chama kwenye uchaguzi
ujao.
Mwenyekiti
wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam,Janneth Masaburi, alisema ziara hiyo
itasaidia kuwajenga kisiasa ili waendane na kasi ya mabadiliko ya ujenzi
wa Chama na kasi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Alisema
Mpogolo amegusa mambo muhimu, ambayo yatasaidia wanachama kufanya
uchaguzi huru na viongozi wa mkoa wataendelea kuelimisha wana CCM ili
kujiimarisha zaidi.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi, alisema Naibu
Katibu Mkuu Mpogolo, anatoa elimu muhimu juu ya dhamira ya Chama ya
kujenga mashina na kuongeza wanachama.
Alisema
ziara hiyo imejenga hamasa na wanachama wameelimishwa kuepuka chuki na
kujenga upendo miongoni mwao jambo ambalo ni muhimu hususan kwa kipindi
cha uchaguzi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akiwasili
kwenye Ukumbi wa Kijichi Mbagala kwa ajili ya kuzungumza na wanachama na
Viongozi wa CCM.
Naibu
Katibu Mkuu, Lodrick Mpogolo akiwasili ukumbini (kushoto) ni Mkubwa
Fela akiwa ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano huo.
Wanachama wa CCM wakiimba wimbo maalum
Akipokelewa na wanachama wa Kijichi
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akisalimiana
na baadhi ya Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika
mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es
Salaam,jana.
Vijana
wa Kikundi cha Hamasa cha CCM Kata ya Mtoni, wakisebeneka wakati wa
mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Lodrick Mpogolo, alipokuwa katika
ziara ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na
wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika
mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es
Salaam,jana.
Baadhi ya Wanachama wa CCM Kata ya Mtoni wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo,
Wazee wa CCM wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Lodrick Mpogolo, katika Ukumbi wa CCM Mtoni.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akiwasili
kwenye Ukumbi wa CCM Mtoni kwa ajili ya kuzungumza na wanachama na
Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara
zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es Salaam,jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (kushoto) akizungumza na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara Lodrick Mpogolo, wakati alipomtembelea ofisini
kwake alipokuwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo la
Temeke jijini Dar es Salaam jana.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Lodrick Mpogolo, akizungumza kutoa shukrani
zake kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala (hawapo
pichani) kwa mapokezi, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha
Chama kwa Jimbo la Temeke jana.
Picha ya pamoja baada ya mazungumzo
Tags
CCM
