Wachezaji watano wameteuliwa (nominees) kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.
Walioteuliwa kuingia kwenye
kinyang’anyiro hicho ni Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima
(Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva
(Yanga).
Majina hayo yatapigiwa kura na
makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom
pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari
nchini.
Wahusika watatumiwa fomu maalum za
kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari.
Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu.
Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo
inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es Salaam.
Tags
MCHEZAJI BORA