Mbunge Nape Nnauye ljana bungeni wakati akichangia katika bajeti ya
Wizara wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema Wanakusini hawatakubali
kuona ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi unakwama kutokana na vita
iliyopo kati ya mataifa makubwa.
Nape Nnauye amemtaka Waziri Mwijage asikubali kuona vita ya mataifa hayo
inaendelea kuwaumiza wananchi wa Kusini na kusema kama atafanya hivyo
wao hawatakubali hilo jambo.
"Mwijage viwanda ni ukombozi hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa
sababu bado ni masikini sana na ukombozi wowote una vita, hasa kwa wale
ambao wanafaidika na mfumo wa kutokuwepo kwa viwanda. Na hapa nitatoa
mfano. Tumekuwa tukizungumza juu ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi,
Kilwa pale ila taarifa tulizonazo mataifa makubwa yenye 'interest' na
mbolea katika nchi hii yanapambana kuhakikisha kiwanda hicho hakijengwi.
Katika jambo ambalo hatutakubaliana nalo Mwijage ni pamoja na hili,
kuruhusu vita hii iendelee kutuumiza wanakusini" alisema Nape Nnauye
Nape Nnauye aliendelea kusisitiza
"Mataifa hayo yanapigana kwa maslahi yao na kama serikali mtayumba
kwenye hili basi Wanakusini hatutokubali, tulishalizungumza,
mlishakubaliana, mwekezaji alishapatikana na utaratibu uko wazi, sasa
vita hii ya wakubwa isituumize sisi wakapiganie nje ya Lindi lakini
tunakitaka kiwanda cha mbolea Lindi" alikazia Nape Nnauye
Tags
Nape Nnauye
