
England.Kufanana na Lionel Messi nusura kumpeleke jela mwanafunzi wa
Kiirani baada ya kuzua vurugu kwa mashabiki waliotaka kupiga naye picha
mitaani.
Mwanafunzi huyo, Reza Parastesh anayefanana na Messi aliwavutia
mashabiki wengi wakiomba kupiga naye picha 'selfies' jambo
lililosababisha vurugu na kulazimisha polisi kumkata na kumpeleka kituo
cha polisi.
Pia, gari la Paratesh (25) liliongozwa na trafiki kutoka katika kituo hicho kutokana na mashabiki wengi wa Iran kuvutiwa naye.
Paratesh alisema: “Sasa watu wananiona mimi kama Messi wa Iran na
wananitaka mimi nifanye kila kitu anachofanya. Ninapojitokea sehemu
yoyote watu wote wanachanganyikiwa.
“Nina furaha sana kuona jinsi ninavyoweza kuwapa furaha watu wengi.”
Parastesh kwa sasa anabadilisha nywele zake na kufanana na Messi na mara kadhaa anapopita mitaani anavaa jezi ya Barcelona.
Tags
MICHEZO