
Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe,amemteua binti yake wa pekee, aliyemaliza
masomo yake nchini Singapore, mwenye shahada ya uzamili katika masuala
ya usimamizi katika mabenki na fedha, Bona Mugabe-Chikore, kuwa katika
bodi ya udhibiti vyombo vya habari.
Bona ameteuliwa kudhibiti vyombo hivyo vya habari ikiwemo na sekta ya
filamu katika nchi hiyo. Naye Charity Charamba, ambaye ni msemaji wa
jeshi la polisi atakuwa moja ya watu katiaka bodi hiyo ya watu 11.
Bodi hiyo ilitangazwa na Waziri wa mambo ya ndani Ignatious Chombo,
ikihusisha wawakilishi wa makundi ya makanisa, wataalamu wa sheria na
uhasibu na viongozi wa kitamaduni. Shirika la kitaifa la habari limesema
bodi hiyo itadhibiti na kukagua vyombo vya habari na sekta ya filamu
nchini na kulenga “matumivi mabaya ya mitandao ya kijamii .
Tags
Robert Mugabe