
Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili, amendika ujumbe
unaoandamana na harakati za Rais Dkt. John Magufuli za kupambana na wizi
wa mchanga wa dhahabu ambao jana amepokea ripoti ya suala hilo.
Kupitia mtandao wa kijamii Nikki ameandika, ‘Watanzania wanaopewa
dhamana, wasipoamua kuwa waadilifu, umaskini utaandika historia tukufu
kwa Tanzania, alafu kuna uhusiano gani kati ya uwekezaji na ufisadi….
maana kila kasha, wizi mkubwa utamkuta mwekezaji na wakala wake wa
kitanzania (wasomi, viongozi, wafanya biashara), yaani ni kama ule
uchumi wa kikoloni manufaa ni kwa makampuni ya nje na kitabaka cha
watanzania wachache.
“Nimpongeze mkuu wa nchi kwa kuamua kupambana na ufisadi huu, ila vita
ya kuvunja mfumo wa kiuchumi wa kifisadi ni hatari, kina Lumumba,
Nkruma, Sankara, huko Chile, Nikaragwa, Venezuela, haiti, Iran….
viongozi hawakupona, ni vita kuu. Mungu akusimamie,” ameandika Nikki.
Tags
Niki wa Pili