Mhe.Prof Makame Mbarawa Waziri wa
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano akishuhudia Utiaji saini mkataba wa kuuza
China bidhaa za muhogo kutoka Tanzania Mkataba huo umesainiwa Jana
mjini
Beijing Jamhuri ya watu wa China kati ya Balozi wa Tanzania nchini China
Mhe.Balozi Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Li Yuanping Naibu mkurugenzi mkuu wa taasisi ya udhibiti
na ukaguzi wa mazao kwa niaba ya Serikali ya jamhuri ya China
Mhe.Mbarawa yupo mjini Beijing ambapo aliwakilisha serikali ya Tanzania
kwenye mkutano wa One belt one Roads Forum.