
Ni mwezi mmoja umepita baada ya Kampuni ya Apple kutangaza kuwa
watajikita katika utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe, tayari
mshindani wake kibiashara kampuni ya Samsung nao wamepata kibali cha
kutengeneza magari hayo.
Samsung wamepata kibali cha kutengeneza magari hayo kutoka kwa Serikali
ya Korea Kusini ambako ndiyo makao makuu ya kampuni hiyo yaliko, huku
wakijinadi kuwa wamefikia uamuzi wa kutengeneza magari hayo kuendana na
teknolojia.
Taarifa kutoka mtandao wa Thenextweb zimeeleza kuwa Samsung wataanza
kwanza majaribio yao na Kampuni ya magari ya Hyundai na baadae
kutengeneza magari yao wenyewe.
“Lengo kubwa la Kampuni yetu ni kuhakikisha dunia inakuwa salama zaidi
sio tu kwa mazingira bali hata viumbe hai ndiyo maana kila kukicha
tunajitahidi kuleta vitu vipya,Teknolojia hii (Magari yanayojiendesha
yenyewe) itasaidia kupunguza msongamano,Kupunguza ajali na kulinda
mazingira“Alisema Afisa mipango wa Kampuni ya Samsung Bw. Young Sohn.
Mwishoni mwa mwaka jana Samsung walinunua kampuni ya HARMAN
inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya ndani vya magari kwa Dola
Bilioni 8 za kimarekani hivyo huenda ilikuwa ni njia ya kujiwekea
urahisi kwa kampuni hiyo kuingia kwenye teknolojia ya magari
yanayojiendesha hivyo tutarajie kuona magari ya kampuni hiyo yenye nguvu
zaidi duniani.
Kwa sasa bei ya magari hayo haijatajwa, kutokana na sababu za kibiashara .
Kampuni ya Samsung itaungana na makampuni mengine makubwa Duniani kama
Tesla, Apple,Google na mengine kibao kwenye ushindani wa soko la magari
yanayojiendesha yenyewe.
Tags
Technology