
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Dk Tao Zhang
amempongeza Rais John Magufuli kwa jitihada zake za kupiga vita
rushwa, ufisadi na ukwepaji kodi.
Dk Zhang amesema uchumi wa taifa lolote unategemea kwa kiasi kikubwa
makusanyo ya kodi kinyume na hapo ni vigumu kufikia maendeleo.
Naibu huyo amesema ili kukabiliana na changamoto za rushwa ni muhimu
vyombo na taasisi za Serikali kuwa imara na kufanya kazi kwa ufanisi.
"Najua hii ni mada nyeti kwa mataifa mengi, ila natumai wote tunafahamu
namna rushwa na ukwepaji kodi vinavyokwamisha kukuza uchumi wa
nchi,"amesema.
Tags
RAIS MAGUFULI