CASHEWNUT
BOARD OF TANZANIA
HEAD OFFICE -
MTWARA
BRANCHES
BRANCHES
P.O. BOX 533 DAR ES SALAAM
Telephone: (023) 2333303 P.O. Box 9234
Fax: (023) 2333536 Telephone: (022) 2113161
Website: www.cashew.go.tz TANGA
P.O.Box065
Telephone (027) 2647304
Fax: (027) 2646850
TUNDURU
P.O. Box 127
Telephone/Fax (025) 2680221
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAKUKURU
kubana wezi Tasnia ya Korosho
Dodoma,
Mei 16, 2017
KUTAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) itafuatiIia na kubana wezi ndani ya
Tasnia ya Korosho ili mkulima apate stahili yake.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU, Velentino Mlowola, amesema kuna wizi na udanganyifu mwingi
ndani ta Tasnia ya Korosho na hivyo wakati umefika sasa wa wabaya wote
kupelekwa mbele ya sheria.
Alikuwa
akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia
ya Korosho, uliofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma ukifunguliwa na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na kuendeshwa na Mwenyekiti wa Wadau, mzee Hemed Mkali.
“
Nimekuzwa na uchumi wa Korosho. Mengine nitakayoyasema hapa nayajua kwa sababu
hiyo, si kwa sababu ya kuyasoma vitabuni tu. Tasnia ya Korosho ni miongoni mwa
sekta muhimu sana katika uchumi wa Taifa letu. Korosho ndilo zao kuu la
biashara katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania. Lakini sekta hii inakabiliwa na
changamoto kadhaa zinazokwaza maendeleo ya sekta yenyewe na uchumi wa wananchi
wanaozalisha Korosho na pia Mapato ya Serikali ambayo hutumika kugharamia
maendeleo ya wananchi na usalama wao. Changamoto zinazoathiri sekta ya Korosho
zinahitaji kuingiliwa kati na Serikali ili wananchi wanaozalisha Korosho wapate
stahili zao na hivyo kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla.
“
Kuna malalamiko mengi kutoka kwa wakulima ambayo mengine yanasababishwa na ukosefu wa uadilifu na
kuwapo kwa rushwa. Migogoro ni mingi kwenye vyama vya Msingi na Vikuu na
inadidimiza dhana nzima ya Ushirika. Na wakulima kutolipwa au kupunjwa fedha za
mauzo ya Korosho baada ya Korosho zote kuuzwa minadani.
“
Kuwapo wa mlolongo wa kodi nyingi zinazotozwa kwenye mauzo ya Korosho mfano;
makato ya usambazaji wa fedha na kinachoitwa
Task Force. Ugumu wa upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na huduma za
Ugani kutosambaa kwa wakulima wengi,” alisema.
Alisema
TAKUKURU imeorodhesha makosa 24, baadhi ya makosa hayo yakiathiri kwa kiwango
kikubwa maendeleo ya sekta ya Korosho.
“
Tunayachunguza katika kutekeleza jukumu letu la kusimamia Sheria katika Sekta.
Kuna mianya mingi ya rushwa kwenye
Korosho kama ununuzi wa Korosho kwa njia za vichochoroni maarufu kwa jina la
“Kangomba” dhidi ya mfumo rasmi uliowekwa. Viongozi wa Serikali za Mitaa
kutojihusisha na jukumu lao la kusimamia taratibu za kiserikali zinazodhibiti
ubadhirifu, (wanaporuhusu biashara ya “Kangomba” kufanyika kwenye maeneo
wanayoyaongoza kuna uwezekano mkubwa wanafanya hivyo kutokana na kuwapo rushwa)
na baadhi ya viongozi wa Serikali na vyama vya Ushirika kuingiza siasa kwenye
zao la Korosho na kusababisha athari kubwa kwa wakulima na wanachama.
Akifungua
Mkutano huo Waziri Mkuu Majaliwa alisema
Serikali ya awamu ya tano italilinda zao la Korosho kwa kufa na kupona.
Naye
Waziri Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba alisema kuanzia msimu huu
dawa ya wadudu ya sulphur itatolewa bure kwa wakulima na kwamba Serikali pia
iko mbioni kugawa bure magunia na vifungashio vya zao la Korosho.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho (CBT) ambayo ndiyo iliyoandaa mkutano huo
uliohudhuriwa na washiriki wapatao 600, Hassan Jarufu, amesema tayari wadau
wamekutana kupanga namna ya kusambaza pembejeo hizo kwa kutumia Kamati za
Pembejeo za Mikoa, Wilaya na Vijiji.
Amesema
pia kwamba Bodi ya Korosho itagawa bure kwa wakulima pembejeo za dawa
zilizobaki katika msimu uliopita badala ya kuziharibu kwa kuwa zoezi hilo la
kuzitekeza ni la gharama kubwa.
Tags
KOROSHO