BANDA MEDIA BLOG

DC AKIFUNGIA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI DODOMA...... AAGIZA MMLIKI KUREJESHEA WANAFUNZI FEDHA ZAO NDANI YA SIKU 7....!!!!!



Chuo cha East Africa College kilichofungwa
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mndeme

Katikati Mkuu wa Chuo cha East Africa College akiwa ofisini kwa mkuu wa wilaya alipokuwa akihojiwa kuhusu malalamiko ya wanafunzi kabla ya kuamuliwa kufunga chuo chake mpaka hapo atakapo kamilisha usajili kulia ni mmoja wa awalimu wa chuo hicho na kulia ni Kamanda wa Polisi Wilaya ya Dodoma mjini [OCD] Daniel Shija [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo hicho wakiwa ofisini kwa mkuu wa wilaya walikofika kutaka serikali iingilie kati kuhusu malalamiko yao
Ripoti ya John Banda, Dodoma

MKUU wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme amekifunga Chuo cha Uandishi wa habari cha East Africa College  huku akimtaka mkuu wa chuo hicho kuwarejeshea wanafunzi ziadi ya 100 ada zao ndani ya wiki moja kutokana na kutokuwa na usajili.

Mndeme amelitoa agizo hilo wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho walioandamana mpaka katika ofisi za mkuu wa wilaya wakitaka usaidizi wa madai yao mbalimbali ikiwemo vyeti vyao baada ya kumaliza

ameutaka uongozi wa chuo hicho kuwarudishia wanafunzi wote wafedha zao za ada na michango mingine katika kipindi cha wiki moja ikiwa ni pamoja kusafisha vyeti vya wahitimu ambao wapo majumbani kwa garama za chuo

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wanafunzi waliosoma na kupata vyeti chuoni hapo kufungua jarada polisi ili hatua za upelelezi zianze kufanyika na ikibainika kuwa mwenye chuo alikuwa akifanya utaperi kwa kutumia cheti cha mandia atachukuliwa hatua kali ikiwemo ya kufikishwa mahakamni

kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Mshukuru Boeboe amesema amekuwa afuatilia usajili wa chuo hicho tangu mwaka 2012 alipokifungua bila mafanikio lakini akahidi kufanya bidii 

"nitafuatilia kwa bidii sana na baada ya muda mfupi nitakifungua chuo changu hivyo wazazi na wanafunzi wasiwe na wasiwasi wowote katika hilo", alisema
Wanafunzi wa chuo hicho Rehema Saimon na Rais wa wanafunzi Twaha Salim Iddy  wakaweka wazi malalamiko yao ikiwemo fedha nyingi wanazotumia na kumbe chuo hakikuwa na usajili

 "ni wiki mbili sasa tangu kuanza kufuatilia ili tupate haki zetu na sasa tunamshukuru Mungu Dc  ametusaidia na tuna imani ya kuzipata fedha zetu ndani ya hiyo wiki moja ili wengine turudi mikoani kwetu , 

tulichanganyikiwa sana baada ya kugungua chuo hakina usajali na kuanza kuwafilia wenzetu ambao tayari walishasoma na kupata vyeti ndiyo maana hawapati mikataba ya kazi hasa waliyopo kwenye maredio bora serikali itusaidie ili baaada e tusije kuutana na tumbua tumbua ya Magufuli", walisema

Chuo hicho kilichopo mailimbili karibu na mnada wa zamani  manispaa ya Dodoma kina zaidi ya wanafunzi 100 wa kozi mbalimbali zikiwemo za uandishi wa habari na utangazaji huku wakilipia 800,000, malipo ya mabweni, nauri na chakula

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG