BANDA MEDIA BLOG

TECNO SAFE YAFANIKISHA MAFUNZO YA UKULIMA, UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UTUNZAJI WA ZAO LA ALIZETI KWA WAKULIMA WA WILAYA YA CHEMBA, ILI KUEPUKANA NA FANGASI ANAYEZALISHA SUMU KUVU




Afsa kilimo wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma Chrisanti Sifunda akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na wakalima wa Alizeti wilayani humo
 

Mafunzo yakiendelea
Mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la 3 Sisters linalojihusisha na usindkaji wa Mafuta ya alizeti, Asali na Alovela Mariamu Majengo akionyesha vitini vya mafunzo ya Ukulima, uandaaji, uvunaji na utunzaji bora wa zao hilo fangasi wanaozalisha sumu kuvu [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]
alizeti zikiwa shambani kabla ya kuvunwa
wakulima wilayani Chemba wakijaza alizeti ilikwishavunwa kwenye mifuko kabla ya kuipeleka sokoni


Mafunzo yakiendelea


mmoja wa wakulima hao akifurahia jambo wakati mafunzo hayo yakiendelea




John Banda, Dodoma
 WAKULIMA Nchini wameshauliwa kuvuna mazao yaliyokomaa, kuyakausha na kuyahifadhi vizuri ili kuepukana na fangasi anayezalisha vilusi vya sumu kuvu ambavyo ni hatari kwa afya ya binamu ikiwemo vifo.

Usahauri huo umetolewa na Afsa kilimo wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma Chrisanti Sifunda wakati akiongea na wakulima wa zao la alizeti wakati wa mafunzo ya kilimo, uvunaji na uhifadhi bora wa zao hilo yaliyoratibiwa na Shirika linasindika mafuta ya alizeti, asali na Alovela la 3 Sisters Chini ya udhamini wa TECNO SAFE
Afsa huyo amewataka wakulima hao kuhakikisha wanazingatia ushauri unaotolewa na wataraamu ikiwemo kuwa wepesi wa kuwafuata na kuwaomba ushauri.

Aidha Sifunda ameyataja madhara yanasababishwa na Sumu kuvu ikiwemo kuvimba tumbo, kuhara, kutapika, macho kuwa ya njano na kama kiwango chake ni kikubwa husababisha vifo

Nae Mwakilishi wa Shirika linalosindika mazao ya Alizeti, asali na alovela la 3 Sister la Mjini Dodoma Mariamu Majengo  ameitaja sumu hiyo kuwa ni hatari kwa mwaka 2016 watu 17 walipoteza maisha katika baadhi ya vijiji wilayani Chemba baada ya  kula nyama ya ng’ombe ambaye alikuwa kala pumba na alizeti iliyokuwa imeathiliwa na Sumu hiyo

Wakulima hawa John Molo na Moringe Kimosa wamesema wamepata ufahamu wa kutosha kuhusu Sumu kuvu ambapo walikuwa wanaona dalili zilizotajwa  bila kujua na wakifahamu kuwa sumu hiyo haifi hata ikipikwa na kutiwa chumvi

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG