Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake
leo Jijini Dar es Salaam.
: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake
leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Majaribio ya Dawa na
Ufuatiliaji kutoka Mamlaka hiyo Bi. Kissa Mwamwitwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Hiiti Sillo (katikati) akifafanua jambo
mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na waandishi
wahabari( hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake
leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kanda ya
Mashariki wa TFDA, Emmanuel Alphonce na Meneja Majaribio ya Dawa na
Ufuatiliaji kutoka Mamlaka hiyo Bi. Kissa Mwamwitwa.
Picha zote na: Frank Mvungi – MAELEZO
…………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imewahakikishia wananchi
kuwa dawa zilizopo katika soko zina ubora kwa asilimia 98 na
itahakiksha zinaendelea kukidhi vigezo vya ubora kama zilivyokuwa wakati
zinasajiliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni,miongozo na taratibu za
udhibiti.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA)
Bw. Hiiti Sillo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga
kueleza mikakati ya Mamlaka hiyo katika kudhibiti ubora na usalama wa
chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya za wananchi.
“Katika maabara ya TFDA
inayokidhi ithibati ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kati ya sampuli za
dawa 199 za Binadamu zilizochunguzwa,sampuli 184 sawa na asilimia 92.5
zilikidhi vigezo vya ubora na sampuli za dawa 10 aina ya Ergometrine ya
sindano ambayo ni sampuli 5 sawa na asilimia 2.5 hazikufikia ubora kwa
kuwa na kiasi cha kiambata hai chini ya kiwango
kinachokubalika.”Alisisitiza Sillo
Akifafanua Sillo amesema kabla ya
dawa kusajiliwa na TFDA na hatimaye kuruhusiwa kuingia katika
Soko,zinafanyiwa tathmini ya Ubora,Usalama na ufanisi sanjari na ukaguzi
wa mifumo ya utengenezaji bora Kiwandani na hizo ni hatua za awali za
mifumo ya udhibiti wa dawa duniani.
Pia Sillo aliongeza kuwa dawa
zinapokuwa katika soko zinafuatiliwa na TFDA kuona kama zinaendelea
kukidhi vigezo vya ubora hadi tarehe ya mwisho ya matumizi (expiry date)
ambapo utaratibu huu hujulikana kama Post- Marketing Surveillance au
Market Control kwa mujibu wa mwongozo wa shirika la Afya Duniani (WHO)
na ulianza kuwekwa na TFDA tangu mwaka 2007.
Katika utaratibu huo kila mwaka
sampuli za dawa za aina tofauti zinachukuliwa na wakaguzi kutoka katika
soko Zahanati,Vituo vya Afya, Hospitali,maduka ya dawa na maghala ya
kuhifadhia dawa ya umma na binafsi na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara.
Vigezo vinavyotumika kuchagua
dawa zinazofanyiwa ufuatiliaji ni pamoja na dawa zenye matumizi
makubwa,dawa za kutibu magonjwa ya makundi maalum kama watoto na akina
mama wajawazito,dawa zenye historia ya kushindwa kustahili mazingira
mbalimbali ya usafirishaji na utunzaji (unstable products)
Kwa kipindi cha mwaka 2012/2015
Sillo alibainisha kuwa dawa zilizofanyiwa ufuatiliaji ili kuona ubora
wake ni pamoja na dawa za kutibu malaria,dawa aina ya vijiua sumu
(Antibiotics) Dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi,dawa za kupunguza
maumivu,dawa za kutibu kisukari,dawa za kutibu magonjwa ya moyo,dawa za
kuzuia kutoka damu nyingi wakati wa kujifungua aina ya misoprostol.
Katika kipindi cha mwaka
2016/2017 hadi machi 2017, TFDA ilifuatilia katika soko,ubora wa dawa za
binadamu aina ya Albendazole vidonge,mchnaganyiko wa dawa ya vidonge
aina ya Diclofenac na paracetamol,dawa ya macho yenye mchanganyiko wa
Dexamethazone na Neomycin,dawa za mifugo aina ya Oxytetracycline 10% na
20 ambazo uchunguzi wake uko katika hatua za mwisho na matokeo
yatatolewa mara yatakapokuwa tayari.
Aidha Sillo amesema kuwa mfumo wa
kufuatilia usalama wa dawa katika soko unafanya kazi vizuri hapa nchini
tangu mwaka 1989 na umeendelea kuboreshwa ambapo oktoba 2016
tulianzisha mfumo wa utoaji taarifa za madhara ya dawa kielekroniki kwa
kutumia simu ya kiganjani.
Mamlaka ya Chakula na Dawa
Tanzania(TFDA) kwa mujibu wa Sheria ya Chakula,Dawa na Vipodozi,sura ya
219 ina jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa chakula,dawa, vipodozi
na vifaa tiba ili kulinda Afya za wananchi.
Tags
TBS