
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umezuka
katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo.
Eugene Kabambie ni msemaji wa WHO nchini humo amesema kuwa shirika hilo
limeanza kuchukua hatua baada ya watu watatu kufariki wakihisiwa kuwa na
ugonjwa wa Ebola. Pia WHO imesema mlipuko huo unaathiri maeneo ya
msituni ya Aketi, katika mkoa wa Bas-Uele karibu na mpaka wa nchi hiyo
na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Waziri wa Afya wa DR Congo, Oly Kalenga kupitia barua, amesema kuwa watu
tisa kutoka eneo la kiafya la Likati, Aketi waliohofiwa kuwa na
Ebola.Watano kati yao walipimwa na mmoja wao akathibitishwa kuwa na
virusi hivyo na watatu walifariki.
Mwaka 2014, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamuhuri ya demokrasia ya
Congo ulidhibitiwa kwa haraka ingawa watu 49 walifariki. Na watu waptao
watu zaidi ya 11,000 walifariki kutokana na mlipuko wa Ebola Afrika
Magharibi 2014-2015, sana nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia katika
mlipuko wa Ebola ulioatajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani.
Mlipuko huo wa sasa ni wa nane kutokea nchini DR Congo tangu mwaka 1976.