
Wakuu katika kuheshimu Mamlaka Viongozi na hasa Viongozi wastaafu wako
nyuma sana mtu unamuuliza kwanini imefanya kitendo hiki hakikubaliki
yeye anakimbilia Kusema "Unajua unaongea na Nani?'' Au "Unajua Mimi
nani?''
Kwanini hutaki kujieleza kama Raia wa Tanzania unayefuata Sheria Ni vema
Kufuata Utaratibu wa Kisheria kuna Askari wengine hata kiumri wadogo
hata hawà jui Kua Lytonga Mrema alikuaga Waziri wa Mambo ya Ndani.
Suala la Parking linaongeleka Mimi mwenyewe huwa nakuta Lim/tairi
limefungwa na Mnyororo lakini najishusha jamaa wanatoa mnyororo halafu
maisha yanaendelea.
Nimechukulia Mfano wa Viral iliyoenea ikimuonesha Malima akitishiwa na
Askari Katika Video ile Nimesikitishwa Kusikia hata Raia wa Pembeni
wakishabikia Unajua unaongea na Nani huyo.
Kitendo hicho ni kumu intimidate askari asitimize wajibu wake
unavyojitambulisha usihojiwe kama Mtanzania Unaeishi kwa Kufuata Sheria
za Nchi.
Siungi Vitendo vya Matumizi ya Silaha ila watanzania tufuate Sheria
ikiwa Pamoja na Kua cha tabia ya Kutishia unajua Unaongea na nani? Yaani
hata Mimi hiyo kauli huwa inaniboa sana.
Tags
Ulweli Mtupu