Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha baada ya taarifa kutoka
serikali kuwa imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa
787-8.
Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.
Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe
za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami
nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.
Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.
1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama
zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2
nakuendelea.
2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8.
Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini
hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi
mapya ili kupata ndege bora zaidi.
Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine.
Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege
zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi
hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344
Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon,
Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege
zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na
kuendelea.
Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi
ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi
toka 2009 zilipoanza tengenezwa.
Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo
(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege
(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)
CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga
zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number
35508, Line number 19.
Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20.
Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa
jina la Terrible Teens.
Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda
,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani
$224.6M?
Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.
Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini
anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa
kazi.
Tags
ndege mpya
