
*Ushauri kwa _Tundu Lisu_*
Ukiwa Kama mwanasheria mashuhuri nakuomba ulisaidie Taifa na hawa
mapepari na majizi ya rasilimali zetu wanaojiandaa kwenda kulishitaki
Taifa letu kwenye Mahakama za kimataifa kisa tu Taifa limechukua hatua
kwa namna tunavyoibiwa rasilimali zetu na hao mabepari wanatumia mgongo
wa sheria tena walizotunga wao na zinabeba hao hao kuendelea kutunyonya
kwa kigezo cha Mahakama za kimataifa.
Ni kweli kutokana na sheria za kimataifa zilivyokaa ikitokea ACACIA
wakaenda mahakamani Taifa litawalipa fidia kubwa sana, pesa ambazo ni
kodi za sisi wananchi wa hali za chini. Ifahamike kuwa hawa wawekezaji
wanatuibia kwa kutorosha rasilimali zetu wakijua mwisho wa siku kuna
sheria za kimataifa zilizotungwa na hao hao zitawatetea tena. Kwa lengo
la kizalendo nakuomba Tundu Lisu Ukiwa Kama Rais wa TLS na pia Mtanzania
mwenzetu andaa timu yako ya wanasheria mahili (Akina Malya, Mabere
Malando, Chenge) na wengine wengi kuhakikisha mnaenda kupambana nao huko
kwenye Mahakama zao wanakopanga kwenda kulishitaki Taifa.
Kwa hili la rasilimali zetu tuweke uvyama pembeni tuungane kumuunga
mkono Mh Raisi kwa hatua alizochukua. Ni kweli kabisa bado Kuna
changamoto nyingi kwenye uwekezani wa rasilimali zetu haswa katika
upande wa mikataba na sheria mbovu zinazosimamia hiyo mikataba
iliyosainiwa na viongozi wetu ambao pia ni Watanzania wenzetu (wengine
bado wapo madarakani eg. Akina Chenge kipindi hicho akiwa mwanasheria
mkuu wa Serikali) .
Hivyo basi kwa hatua za awali hawa wanaojiita wawekezaji tukiwashinda
kwa hili la mchanga hayo mengine ya mikataba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu
siku moja pia tutayafikia tu.
*UKWELI HUWA UNA ASILI YA KUUMIZA, ILA KWA HILI LA RASILIMALI ZETU TUSIMAME UPANDE WA UKWELI*
Chanzo jf
Tags
tundu lissu