BANDA MEDIA BLOG

ZAIDI YA WATU 23 WAMEUWAWA JAMII YA KIKRISTO NCHINI MISRI


Cairo: Nchini Misri kumetokea mauwaji ya zaidi ya watu 23 ambao wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kufyatulia risasi waumini wa kanisa la Coptic waliokuwa wakisafiri kwa kutumia basi katikati mwa Misri, vyombo vya habari vya serikali ya nchini Misri vemeripoti.

Tukio hilo limetokea katika mkoa wa Minya,ambapo ni zaidi ya takriban km 250 kusini mwa Cairo, basi hilo lilipokuwa linawasafirisha waumini hau kwenda kanisani.


Hivi karibuni Kumetokea visa kadha vya waumini wa kanisa la Coptic kushambuliwa, mashambulio ambayo kundi la Islamic State limedai kuhusika.
Mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa mhanga katika makanisa Tanta na Alexandria mnamo 9 Aprili yalisababisha vifo vya watu 46.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG