SERIKALI Mkoani Dodoma imewatahadharisha wananchi wa Dodoma na nje ya Dodoma
ambao wameanza kuvamia maeneo mbalimbali katika manispaa ya dodoma
kuondoka mara moja vinginevyo serikali haitawavulimia kwani wanaenda
kinyime cha sheria.
Pia serikali imesema kuwa kuanzia sasa kwa Mkoa wa Dodoma ni marufuki mtu kugawa shamba lake au eneo lake bila kufuata taratibu za kitaalamu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordani Rugimbana wakati akifunga mafunzo ya chama cha wapimaji wa ardhi nchini (IST) yaliyofanyika mkoani hapa yakiwa na lengo la kuwapa elimu wapimaji wa ardhi ili kuweza kufanya kazi zao kwa kukidhi mahitaji ya soko na mahitaji ya nchi
.
Hata hivyo Rugimbana amesema kuwa uvamizi huo umeanza baada ya Rais dkt.John Magufuli kuivunja Malmka ya ustawishaji makoa makuu (CDA).
Aidha Rugimbana amesema kuwa anataka baada ya siku chache akae meza moja na uongozi wa Taasisi ya upimaji ardhi nchi [IST]ili kuangalia namna watakavyofanya ili kuendelea kuibadilisha Dodoma.

Kwa pande wake Rais wa IST Martin Chodowa amesema kuwa wao kama wapimaji ardhi watahakikisha wanashirikiana na serikali katika kuhakikisha wanafanikisha zoezi la kupima ardhi.
Ili kuhakikisha kuwa yote hayo yanafanikiwa serikali ya mkoa wa dodoma inatarajia kuaka meza moja na uongozi wa IST ili kupanga kufanya operesheri ya kuifanya dodoma na tanzania kwa ujumla kuwa katika mazingira mazuri zaidi.

Tags
ARDHI