TANZANIA imeingiza
kiasi cha Dola za Kimarekani 301 hadi kufikia Dola Bilioni 1.17 katika
kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 2007 hadi kufikia mwaka 2016.
Hayo yameelezwa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu waziri wa Mambo ya nje na ushirikkano wa Afrika Mashariki, SUZAN KOLIMBA,wakati alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Malindi,SALEHE ALLY SALEHE,aliyetaka kujua Tanzania kama mwanachama wa jumuiya ya nchi za maendeleo kusini mwa Afrika,( SADC) imenufaikaje na soko la Afrika mashariki katika kipindi cha, uanachama wake.
Alisema Tanzania imekuwa ikinufaika na fursa ya soko katika maeneo ya maslahi katika jumuiya hiyo ambayo ni katika maeneo ya viwanda,migodi na madini ambayo yatachangia ukuaji wa kanda toka asilimia nne hadi saba ikiwa ni pamoja na kuongeza pato la taifa toka asilimia 30 katika uzalishaji wa bidhaa kwa teknolojia ya kisasa ifikapo mwaka 2030,kuongeza mchango wa mauzo.
Hata hivyo alisema kuwa Tanzania inanufaika na miradi ya SADC ikiwemo mpango kabambe wa maendeleo ya miundombinu ya nishati ya umeme ya nchi za Zambia na Kenya unaounganishwa toka Tunduma
Pia Tanzania itanufaika na miradi mbalimbali ya uzalishaji katika jumuiya hiyo ya SADC inayounganisha nchi wanachama pamoja na kuongeza ajira

Tags
Dola Bilioni 1.17