TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MEI 24, 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe leo Jumatano Mei 24, 2017
ataongoza viongozi na wanafamilia wengine wa michezo hususani mpira wa
miguu kuilakini Serengeti Boys – timu ya soka ya Tanzania ya Vijana
wenye umri wa miaka 17.
Serengeti Boys inatarajiwa kutua
Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania
leo saa 8:50 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini
ikitokea Libreville, Gabon kupitia Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Mara baada ya kutua, timu
itakwenda Hoteli ya Urban Rose kupata mapumziko angalau ya siku moja
kabla ya TFF kuandaa utaratibu wa kuagana nao.
Baada ya Mheshimiwa Waziri Dk.
Mwakyembe kuthibitisha kutokea Uwanja wa Julius Nyerere kuilaki timu,
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema: “Tunamshuru sana Mheshimiwa Waziri
kwa kuwapokea vijana ambao sasa wanaunda kikosi kipya cha taifa cha
vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
“Kauli mbiu yao – ‘Ngorongoro
Heroes kunyaga twende mpaka kufuzu fainali za AFCON u 20 mwaka 2019’,
michezo ya kufuzu kwa hatua hiyo ya fainali za U-20 zitaanza Aprili,
mwakani. Vijana hawa wataingia kambini tena mwezi Oktoba, mwaka huu na
watacheza mechi ya kimataifa ya kujipima nguvu.
“Mpira huwa haulali, unachezwa saa
24 katika wiki duniani ambako huanzia Januari hadi Desemba,
likimalizika shindano hili linakuja jingine. Maumivu ya kufungwa huwa ni
mafupi, mashabiki siku zote huwa wanafkiria mechi ijayo. Tujiandae na
Qulifiers za 2019 AFCON u-20, haziko mbali.” amesema.
Timu hiyo ya vijana ilikuwa jijini
Libreville nchini Gabon kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
ya vijana iliyofanyika katika miji miwili ya Libreville na Port Gentil
ambako iliondolewa kwenye hatua ya makundi na Niger.
Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0
na Niger katika mchezo uliofanyika Port Gentil, hivyo kufanya matokeo ya
timu zote mbili yaani Niger na Tanzania kufanana kwa pointi, idadi ya
mabao ya kufunga na kufungwa tangu kuanza kwa fainali hizi za AFCON, Mei
15, mwaka huu.
Serengeti Boys iliyokuwa Kundi B
iliondolewa Kundi B iliondolewa na Niger iliyopenya kwenda hatua ya Nusu
Fainali kwa faida ya kupata ushindi katika mchezo ambao umekutanisha
timu hizo kwani Tanzania ilifungwa 1-0 katika mchezo wa mwisho hatua ya
makundi.
Kanuni hiyo ya mashindano ya CAF
inajieleza kuwa matokeo ya ‘head to head’ kwa maana zinapokutana timu
mbili zenye uwiano wa pointi na magoli matokeo huamualiwa kwa mshindi
kupewa nafsi katika mchezo uliokutanisha timu hizo mbili.
Tags
SERENGETI BOYS