Mhandisi wa mitambo ya kusoma
Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja
akieleza matumizi ya kifaa cha kupima mvua kwa Maafisa kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu walipotembelea vituo hivyo vinavyotekelezwa na Mradi wa
Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari uliopo Lushoto
Mkoani Tanga Juni 6, 2017.
Mhasibu Mwandamizi Ofisi ya Waziri
Mkuu Bi. Consolata Mazigo akiuliza swali kwa Mhandisi wa mitambo ya
hali ya hewa Bw. Michael Minja wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi
wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari wa Ofisi
ya Waziri Mkuu Juni 6, 2017 Lushoto Tanga.
Mhandisi wa mitambo ya kusoma
Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja
akieleza matumizi ya mtambo wa kisasa wa usomaji wa taarifa za hali ya
hewa kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa
ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na
Mifumo ya Tahadhari ulio chini ya Ofisi hiyo.
Baadhi ya Watumishi Ofisi ya
Waziri Mkuu wakinukuu maelezo ya Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw.
Vendelin Basso (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kutathimini
Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya
Tahadhari katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Kilimanjaro, wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri
Mkuu (bajeti) Bi. Grace Moshi Juni 7, 2017.
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Mto
Pangani Bw. Vendelin Basso akiwasilisha utekelezaji wa Mradi wa
Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kwa upande wa
Bonde la Mto Pangani mkoani Kilimanjaro wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji
wa mradi huo uliofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 7, 2017.
Mratibu Taifa wa Mradi wa
Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel
Alfei akiwasilisha mada yake wakati wa mkutano wa kutathimini
Utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa Bonde la Mto Pangani Mkoani
Kilimanjaro Juni 7, 2017.
Fundi Sanifu Hydrojia kutoka
Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw.Paul Damian akimuonesha Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Grace Moshi kifaa cha
kusafirisha taarifa za kuongezeka au kupungua kwa maji mtoni (Intelligent Top Cap)
wakati wa tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za
Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Juni 7, 2017 Mkoani Kilimanjaro.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiangalia namna ya Kifaa cha kupima joto Ardhi (Themometer) ikiwa
ni moja ya kifaa kilichofungwa katika Utekelezaji wa Mradi wa
Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari eneo la
Lyamungu Wilayani Hai.
Msaidizi wa masuala ya Hali ya
Hewa Bw. Mbaraka Shaghira (katikati) akieleza matumizi ya Kifaa cha
kupima upepo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea
Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari ili
kuona Utekelezaji wake eneo la Kituo cha Tafiti cha Lyamungu Wilayani
Hai.
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la mto
Pangani Bw. Vendelin Basso akionesha namna ya kusoma kifaa cha kupima
kina cha maji kwa Mchumi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu
Bi. Bivelyne Muchumbuzi kilichopo katika Mto Malala wakati wa ukaguzi wa
Utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya
Tahadhari chini ya Ofisi hiyo Juni 7, 2017
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)