
Msanii wa Bongo Fleva, Jay Moe ameeleza changamoto alizokumbana nazo
shule hadi kupelekea kutoa albamu ya Ulimwengu Ndio Mama, licha ya hiyo
kuna vitu ambavyo anajivunia ikiwemo kusoma shule moja na Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila.
Rapper huyo amesema kutokana na kukulia maisha ya kishua hadi unafika
wakati ambao anaenda boarding school alikuwa hajui kama kuna nyumba za
udongo nchini zaidi ya kuziona kwenye movie za Vietnam.
Ameeleza kuwa wakati anaenda Mbeya kuanza form one mwaka 1993 ndipo
alianza kuona nyumba za udongo kitu kilichomfanya kuanza kulia lakini
baba yake na ndugu zake walipomueleza kuwa amekua hivyo hana budi
kuachana na mambo ya kitoto na kupambana.
“Siku ya kwanza nilipofika Irambo (secondary) jamaa wameniibia begi la
mamisosi, kwa hiyo kule ndipo nilipojifunza maisha kiasi kwamba
nilipofika form three mzee wangu alitaka anihamishie Dar es Salaam
lakini ikamwambi hapana mimi nabaki, nimeshazoea ingawa maisha ni
magumu,” Jay Moe amekiambia kipindi cha The Play List cha Times FM.
Tags
Jay Mo