Kaimu Hakimu Mkazi-Mfawidhi,
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Njombe, Mhe. Paul Kapokolo akiwa ofisini kwake
mkoani Njombe, Mhe. Kapokolo ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Wilaya Njombe amesema Mahakama mkoani Njombe imejiwekea
mikakati ya kushughulikia mashauri kwa wakati ikiwa ni pamoja na kufanya
vikao vya kusukuma mashauri (case flow management) ili kupata ufumbuzi
kwa mashauri yanayoonekana kukwama, kuhimiza Waendesha Mashitaka/Polisi
kuleta mashahidi kwa kila tarehe wanayopangiwa kusikiliza mashauri n.k
Mtendaji, Mahakama ya Hakimu
Mkazi-Njombe, Bi. Maria Francis Itala, Bi. Itala alisema kuwa Mahakama
mkoani Njombe wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa Watumishi wa
Kada mbalimbali, alisema kwa sasa Mkoa huo una jumla ya Watumishi 78 na
uhitaji wa Watumishi ili kutekeleza Majukumu tofauti tofauti ni 359, na
hivyo kufanya kuwa na upungufu wa Watumishi 28.
Muonekano wa jengo la Mahakama
ya Mwanzo Makambako lililopo mkoani Njombe, hali ya miundombinu ya
Majengo katika mkoa huu inaridhisha kwa wastani ingawa kuna baadhi ya
maeneo ambayo majengo yake yanahitaji kufanyiwa ukarabati au kujengwa
kutokana na kutokuwepo kwa majengo kabisa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya Godfrey (kushoto) akiwa katika
ukaguzi maalum alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Kalenga-Iringa ili
kujionea hali ya utendaji kazi katika Mahakama hiyo.
Moja ya vitu alivyokagua
Hakimu huyo Mfawidhi, Mhe. Kalenga ni pamoja na Rejesta ya Mahakama ya
Mwanzo Kalenga kuangalia kama rekodi zinajazwa vizuri kulingana na aina
ya kesi zinazofunguliwa.
muonekano wa jengo la
Mahakama ya Mwanzo Kalenga- Iringa ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya-Iringa amefanya ukaguzi
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakma
ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya alipomaliza kusaini kitabu cha wageni
pindi alipowasili katika Mahakama ya Mwanzo Kalenga kwa ajili ya ukaguzi
wa Mahakama hiyo.
Mhe. Isaya, wa kwanza kulia
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya
Mwanzo-Kalenga, wa kwanza kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya
Mwanzo-Kalenga, Mhe. Magdalena Malaba.
Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya Godfrey akiwa katika picha ya
pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Kalenga mara baada ya
kukamilisha shughuli ya ukaguzi iliyompeleka katika Mahakama hiyo.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama
Tags
Mahakama