
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa uamuzi wa kumvua
uenyekiti uliochukuliwa na chama chake cha ACT-Wazalendo, umefanyika
mapema.
Mghwira ameyasema hayo leo Alhamisi katika Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro mjini hapa, mara baada ya kutia saini kitabu cha wageni.
Hata hivyo, RC huyo mpya amesema hatua hiyo itampunguzia mzigo na
kumrahisishia kazi tofauti na angeendelea kutumikia uenyeketi wa chama
huku akiwa mkuu wa mkoa kwa wakati mmoja.
Mghwira ambaye alikuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo na mgombea wa urais
kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia chama hicho, aliteuliwa hivi
karibuni na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
"Mimi siyo mpinzani wa maendeleo nimepewa jukumu la kutekeleza maendeleo ya nchi," amesema Mghawira.
Tags
anna mghwira