
Hii imenitokea tarehe 28/05/2017 maeneo ya ubungo
Iko hivi hawa jamaa waendesha bodaboda wamebuni mbinu mpya za kuwaibia wateja wao.
Niipanda Boda Boda pale ubungo river side baada ya kumweleza naelekea
wapi nikapewa kofia (helmet) nikavaa ,baada ya kuivaa mara moja dereva
alianza safari na akawa anaendesha mbio ilikuwa jioni ya saa 1:30 kwenda
saa mbili usiku.
Kitendo cha kusogea mbele kidogo nilianza kuishiwa nguvu huku Dereva
naye akianza kupotelea machochoroni baada ya muda mfupi nilipoteza
fahamu sikuwa najitambua tena .
Ilinichukua masaa kama matatu hivi kuja kuzinduka kutoka
usingizini,wakati huo nilijikuta vitu vyangu vyote nilivyobeba sikuwa
navyo ikiwa ni pamoja na pesa kiasi cha shs 180,000 pamoja na laptop
yangu na vitu vingine .
Hivyo nawaonya mnaopanda bodaboda muwe makini hasa nyakati za usiku
helmet Inapakwa madawa yanayosababisha kuishiwa nguvu kabisa na hii
haijalishi mwanamke ,mwanaume kuweni makini na madereva msiowajua.
Tags
Boda Boda