
Marehemu Mzee Ndesamburo kama almaarufu kama Ndesa Pesa, ni watu
waliojiondoa CCM mara baada ya vyama vingi kuanza rasmi nchini Tanzania,
huku akiwa muasisi na mwenyekii wa kwanza wa Chadema mkoa wa
Kilimanjaro. Alikijenga chama huku Sumaye akiwa waziri mkuu alitamka
kejeli akiwa katika ziara mkoani Kilimanjaro miaka ya mwanzoni 2000 kuwa
''ukitaka biashara yako ifanikiwe jiunge na CCM''.
Ndesamburo alitumia rasilimali zake na ushawishi kuijenga Chadema katika
kipindi chote hicho bil kuchoka, Huku akiwa Mwenyekiti wa Mkoa alikuwa
pia mjumbe wa Baraza kuu la chama Taifa hivyo kimadaraka ndani ya chama
ni 'mzito' kuliko akina Lowassa na Sumaye ambao kimsingi walikuja
kugombea uraisi na si kuijenga Chadema.
Haikuwahi kutokea katika uhai wake Mzee ndesamburo kukaa meza kuu lakini
ghafla wajumbe wapya wawili wasio viongozi wa sekretariet wanaketi meza
kuu huku Mzee Ndesamburo akiketi viti vya nyuma kabisa.
Upumzike kwa amani Mzee wangu Ndesamburo, Leo kila mtu anataka kupata
sifa na umaarufu kupitia msiba wako wakati walikutenga kipindi cha uhai
wako.
Chanzo JF
Tags
ndesamburo