Ofisa
Mradi wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ kutoka Shirika la Equality for Growth
(EfG), Suzan Sita (kulia), akitoa mada katika Warsha ya Siku tatu ya
kuwajengea uwezo viongozi wa Umoja wa Wanawake Masokoni iliyohusu
ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa na shirika hilo
inayoendelea katika Hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es Salaam jana.
Viongozi hao wakiwa katika warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Warsha hiyo. Kulia ni Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Irene Daniel.
Taswira katika ukumbi wa mikutano.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa akichangia mada.
Mwezeshaji
Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas, akichangia
mada. (kulia) ni Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha
Juma na kushoto ni Verdiana Gervas kutoka Soko la Ilala.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Ilala Mchikichini, Bupe George akichangia mada.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Kigogo Kisambusa, Mariam Rashid akichangi mada.
Mfanyabiashara kutoka Soko la Gongolamboto, Elika Mwakyusa akichangia.
Mwezeshaji Sheria katika Soko la Temeke Sterio, Johanitha Katunzi akichangia mada.
Mshiriki wa warsha hiyo akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Kiwalani Kigilagila, Bisura Juma akichangia jambo.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
VIONGOZI
Wanawake katika masoko jijini Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk.John
Magufuli atembelee masoko wanayofanyia shughuli zao ili aone changamoto
ya miundombinu katika masoko hayo.
Mwito huo
ulitolewa Dar es Salaam jana na Mwezeshaji wa Sheria katika Soko la
Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas wakati akichangia mada kwenye
warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa umoja wa wanawake
masokoni iliyohusu ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa
na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Alisema
wafanyabiashara wakiwemo wanawake wamekuwa wakilipa ushuru kila siku
katika masoko hayo lakini manispaa husika zimeshindwa kuwajengea
miundombinu kama vyoo bora, umeme na maji hivyo kuwa changamoto kubwa
kwao.
“Tumekuwa
tukitoswa ushuru wa shilingi 500 kwa siku kwa kila mfanyabiashara
lakini hatuoni jitihada zozote zinazochuliwa na hizi manispaa zetu za
kutuwekea miundombinu bora ndio maana tunamupomba Rais wetu afanye ziara
katika masoko tunayofanyia kazi ili tuzungumze naye na kuiona
changamoto hii tuliyonayo” alisema Cleophas.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake wafanyabiashara masokoni Tanzania, Betty Mtewele
alisema wakati ufike manispaa ziweke wazi sheria ya ulipaji wa ushuru
kwa mfanyabiashara ambaye hakufika sokoni kwa zaidi ya miezi miwili
kutokana na kuumwa kwani anapo pona na kurudi katika eneo lake la kazi
anatakiwa kulipa ushuru wa muda huo wote ambao hakufanya biashara wakati
alipokuwa akijiuguza.
“Tunaomba manispaa zetu ziweke wazi jambo hili kwani limekuwa ni changamoto kubwa sana kwetu” alisema Mtewele.
Mwezeshai
wa Sheria katika Soko la Kigogo Sambusa Mariam Rashid alisema zabuni za
uzoaji taka katika masoko zinapaswa kuangaliwa kwa karibu kwani wengi
wanaozipata hawana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo kusababisha masoko
mengi kuwa na changamoto ya mlundikano wa takataka ambapo alishauri
kuondoa mfumo dume katika masoko unaotoa tenda hizo na badala yake
zitolewe fursa kwa wanawake ili waweze kuingia katika kamati za masoko
ili nao waweze kuchangia katika mambo mbalimbali.
Elika
Mwakyusa aliomba manispaa ya Ilala kutenga eneo la soko Gongolamboto
ambako hakuna soko kwani eneo wanalofanyia biashara zao ni la mtu
binafsi hivyo wamekuwa na changamoto kubwa ikiwemo kumlipa ushuru mkubwa
mtu huyo.
Mwezeshaji
sheria wa Soko la Vingunguti wa Simba, Maimuna Mungi alisema
ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi mbalimbali katika soko hilo
hakuna kutokana na kuwepo kwa mfumo dume jambo ambalo limechangia
wanawake wafanyabiashara katika soko hilo kushindwa kuzipatia kusaidiwa
changamoto walizonazo.
Mwezeshai
Sheria kutoka Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa aliomba asilimia
10 ya fedha za makusanyo ya ushuru zibaki katika masoko husika ili
zisaidie ujenzi wa miundombinu.
Ofisa
Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG Suzan Sitha alisema lengo la
warsha hiyo ni kuwaongezea uelewa viongozi wanawake masokoni kuhusu
ukatili dhidi yao pamoja na kupanga mikakati ya kuendeleza kampeni za
kupunguza ukatili dhidi ya wanawake masokoni baada ya mradi kuisha.
Alitaja
lengo lingine ni kutambua haki za wanawake na wahanga wa ukatili dhidi
ya wanawake pamoja na kuwakumbusha viongozi juu ya wajibu wao na
utunzaji wa kumbukumbu za vikundi.
Sitha
alisema warsha hiyo imewashirikisha viongozi wanawake kutoka masoko ya
Manispaa ya Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam, ambayo ni Ilala Boma,
Gongolamboto, Mombasa, Kiwalani, Mchikichini, Kigogo Fresh, Kigogo
Sambusa, Chamazi, Kiustu, Kinyerezi, Feri, Temeke Sterio, Buguruni,
Gezaulole, Tabata Muslim na Vingunguti kwa Simba.
Alisema
karibu changamoto zote zilizopo katika masoko zinalingana kubwa ikiwa ni
miundombinu mibovu licha ya wafanyabiashara kulipa ushuru na kuwa
mradi huo wa Mpe Riziki Si Matusi upo katika Wilaya ya Temeke na Ilala
jijini Dar es Salaam ambapo mradi mkubwa wa Sauti ya Mwanamke Sokoni
upo katika mikoa tisa hapa nchini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
Tags
Masoko Miundombinu