Kocha Msaidizi wa timu ya taifa
ya Tanzania, Fulgence Novatus, amesema kwamba Taifa Stars inayodhaminiwa
na Bia ya Serengeti ya SBL haikuwa na bahati katika mchezo dhidi ya
Amavubi ya Rwanda uliofanyika Uwanja wa Kigali ulioko kata ya
Nyamirambo.
“Tumecheza vema, tulitafuta
nafasi za kutosha. Tumeshambulia sana na kumiliki mpira. Lakini kila
tulipojaribu kufunga, bahati haikuwa kwetu,” amesema Novatus mara baada
ya mchezo huo.
Matokeo ya sare tasa ya jana
yanawapa nafasi ya kusonga mbele Rwanda baada ya sare ya 1-1 katika
mchezo uliofanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza.
Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu
kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi
za ndani (CHAN) na sasa Rwanda itacheza na Uganda mwezi ujao.
Pamoja na kushindwa kusonge
mbele, Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, imeendeleza
rekodi yake ya kutopoteza mechi baada ya kucheza mechi 11 za kimataifa
na kushinda mitano; kutoka sare mitano na kufungwa mmoja wa nusu fainali
za Cosafa.
Tags
Taifa Stars