Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza katika Mkutano wa Wajasiriamali Wilaya ya Mkuranga juu ya kujiwezesha kiuchumi kutokana na ardhi walio nayo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na wanawake
wajasirimali wa Mkuranga juu fursa zilizopo katika Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkurnga, Abdallah Ulega akizungumza na wanawake wa Wilaya hiyo juu kutumia maada za mkutano katika kuzifanya fursa.
Mkurugenzi
wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde (wa kwanza kulia )akisalimiana na
Mwenyekiti wa Jukwa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga, Mariam Abdallah,
katika Mkutano wa Wajasiriamali mkoani Pwani.
Sehemu ya Jukwa la wanawake walikuwapo katika mkutano huo ulifanyika Mkuranga.
…………………………………………………………………………………
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amewatahadharisha wananchi wa
wilaya hiyo kuacha kuuza ardhi hovyo na badala yake kuyatumia maeneo
hayo katika kufanya shughuli za uchumi.
Mkuu
wa Wilaya aliyasema wakati wa Mkutano wa Wanawake 402 Jukwaa Wanawake
wa Wilaya ya Mkuranga ulioandaliwa na Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji
Kiuchumi , amesema
kuwa wananchi wa Mkuranga wakiitumia ardhi vizuri itawapa maendeleo na sio kuuza na kwa ajili ya kucheza ngoma.
kuwa wananchi wa Mkuranga wakiitumia ardhi vizuri itawapa maendeleo na sio kuuza na kwa ajili ya kucheza ngoma.
Amesema
Mkuranga ina ardhi ya kutosha yenye rutuba lakini wananchi wanashindwa
kuitumia katika kujiletea maendeleo na kufanya kuwa na maisha magumu
ya kujiendeesha kiuchumi.
Aidha
amesema mkutano wa wanawake wajasiriamali uwe chachu katika kuanza
kuitumia ardhi katika shughuli za kilimo na mazao watayoyalima
watapata masoko.
Nae
Balozi wa Heshima wa Sheli sheli, Maria Paul amesema kuwa wanawake
walime matunda Passion na Nanasi na kuweza kuyanunua mwenyewe hivyo
hawatakuwa na usumbufu wa soko kwa matunda hayo.
Maria
amesema kuwa wananchi wa Mkuranga wamepata bahati ya ardhi lakini ardhi
hiyo haitumiki katika kuwapa maendeleo wakiwemo wanawake wa wilaya
hiyo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wajasiriamali Wilaya ya Mkuranga, Mariam Abdallah amesema
wakati wa maendeleo umefika wakutumia ardhi katika kuwaletea maendeleo.
Kwa
Upande wa Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa kuna
maendeleo yamewafikia wananchi iliyokuwa changamoto ikiwemo maji
ambapo visima nane vimechimbwa katika vijiji vya Kimazichana Magharibi,
Mkerezange, Midimuni,Ngole , Mwanambaya ,Yava
yava pamoja na Mlaleni.
yava pamoja na Mlaleni.
Aidha
Mbunge ameomba kwa Mkuu wa Wilaya kutumika kwa Kituo cha Mti Pesa kwa
abiri kushuka na kupanda ikiwa na biashara katika mida jioni ambapo
Mkuu wa Wilaya alikubali na kusema jumatatu kituo hicho kitatumika.
Amesema
kuwa vijiji vyote vitapata umeme katika mradi umeme vijiji awamu ya
tatu na upande barabara ya lami kutoka Mkuranga Mjini kwenda Hospitali
ya Wilaya Kupitia ofisi ya Mkuu wa
Wilaya hadi Halmashauri.
Wilaya hadi Halmashauri.
Ulega
ameomba barabara Vikindu Viazi hadi Marogoro, Sangatini pmoaja na
Barabara ya Kiguza , Hoyoyo , Kitonga kuingia katika barabara za Mkoa
ili kutokana na fursa za maendeleo ya maeneo hayo.
Tags
Uchumi